Skip to main content

Huduma za lugha - Kiswahili (Swahili)

Nyenzo zilizotafsiriwa

Tafsiri ya kivinjari (Chagua kichupo)

Idara ya Jimbo la Michigan haiwajibiki kisheria kwa uharibifu au madhara yoyote yanayoweza kusababishwa na matumizi ya tafsiri zozote zinazotolewa na programu au kivinjari cha wahusika wengine. Matumizi ya huduma yoyote ya muhusika mwingine itakuwa ni hiari ya mtumiaji pekee. Taarifa zinazohusiana na huduma za wahusika wengine hutolewa kama zinafaa pekee.

Safari hutoa tafsiri katika Kiarabu, Kichina (Kilichorahisishwa), Kifaransa, Kijerumani, Kiitaliano, Kijapani, Kikorea, Kireno, Kirusi, na Kihispania.

Eneo-kazi (desktop)
1. Fungua kivinjari cha Safari na uchague Vie, kisha Tafsiri kwenye menyu kunjuzi.
2. Weka kivinjari chako katika lugha inayopendelewa, ambayo si Kiingereza.
3. Nenda kwenye ukurasa wa tovuti unaotaka kutafsiri.
4. Kitufe cha kutafsiri kitaonekana upande wa kulia wa upau wa anwani. Huenda tafsiri zisipatikane kwa kurasa zote.
5. Chagua kitufe cha kutafsiri na lugha unayoipendelea.

iPhone au iPad (iPhone or iPad)
1. Fungua kivinjari cha Safari kwenye kifaa chako cha mkononi na uende kwenye ukurasa wa tovuti unaotaka kutafsiri.
2. Chagua alama ya "aA" iliyo karibu na upau wa anwani ili kuona machaguo ya tovuti. Kwenye menyu kunjuzi, chagua Tafsiri kuwa na lugha unayopendelea.
3. Chagua Washa Tafsiri ikiwa menyu ibukizi itaonekana. Kumbuka kwamba utaombwa kuwasha tafsiri mara moja pekee.
Vifaa vya Apple vyenye mifumo endeshi ya zamani zaidi ya IOS 14.0, haitajumuisha kipengele hiki. Pakua programu ya Google Translate au programu ya Microsoft Translator kwenye kifaa chako ili kupata tafsiri.

Eneo-kazi (desktop)
1. Fungua kivinjari cha Chrome na uende kwenye ukurasa wa tovuti unaotaka kutafsiri. Menyu ibukizi ya Tafsiri ya Google inaweza kuonekana chini ya upau wa anwani.
2. Chagua lugha unayoipendelea kwenye menyu ili kutafsiri ukurasa huo.
3. Ikiwa menyu ya kutafsiri haionekani, chagua kitufe cha Google Translate kilicho upande wa kulia wa upau wa anwani. Chagua lugha unayoipendelea kwenye menyu ili kutafsiri ukurasa huo.
4. Ili kupata lugha nyingi zaidi kwa ajili ya tafsiri, chagua kitufe cha Google Translate kilicho upande wa kulia wa upau wa anwani, kisha chagua alama ya menyu ya kitendo.
5. Kwenye menyu kunjuzi, teua Chagua Lugha Nyingine na uchague lugha unayopendelea kwenye menyu kunjuzi.

Simu au kishikwambi cha Android (Android phone or tablet)
1. Fungua kivinjari cha Chrome kwenye kifaa chako cha mkononi na uende kwenye ukurasa wa tovuti unaotaka kutafsiri.
2. Menyu ya Tafsiri ya Google inaweza kuonekana chini ya skrini.
3. Chagua lugha unayoipendelea kwenye menyu ili kutafsiri ukurasa huo.
4. Ili kupata lugha nyingi zaidi za kutafsiri, chagua alama ya menyu ya vitendo na uchague Lugha Zaidi kisha chagua lugha unayoipendelea kwenye menyu kunjuzi.

 
  1. Unapofungua kivinjari cha Microsoft Edge, chagua nukta tatu kwenye kona ya juu kulia ya kivinjari chako kisha, chagua Mipangilio kwenye orodha kunjuzi.
  2. Chagua Lugha, upande wa kushoto wa dirisha la kivinjari chako na uweke lugha unayoipendelea kwa kuchagua Ongeza lugha na kufuata vidokezo.
  3. Ukitembelea ukurasa ambao haujatafsiriwa katika lugha unayoipendelea, menyu ibukizi ya tafsiri inaweza kuonekana kwenye upau wa anwani.
  4. Fuata vidokezo ili kuchagua lugha unayoipendelea na uchague Tafsiri ili kutafsiri ukurasa huo.

 

 

Shughuli za huduma za Katibu wa Jimbo

  • Ukalimani wa Kuchaguliwa kwenye Tawi

    Ofisi za matawi yafuatayo zinatoa huduma za ukalimani kwa njia ya simu. Unaweza kuomba huduma hizi wakati wa miadi yako. Taarifa au ombi la mapema kwa mkalimani sio muhimu. Kwa msaada tafadhali tuma barua pepe kwa MDOS-Access@Michigan.gov.

    Majaribio ya Huduma za Ukalimani

    Iwapo unahitaji kufanya majaribio, kuhudhuria kikao cha kurejeshewa leseni, au kukamilisha uchunguzi mpya wa leseni, lazima utumie mkalimani ambaye ameidhinishwa na Idara ya Jimbo la Michigan kabla ya miadi yako iliyopangwa.

    Unaweza kumuomba mtu yeyote atafsiri kwa niaba yako kwa huduma zingine zote za Katibu wa Jimbo na ziara za ofisi.

    Wakalimani wa kudumu wanaojitolea

    Taarifa kuhusu wakalimani wa kudumu walioidhinishwa inapatikana kwa kupiga simu 888-SOS-MICH (888-767-6424) au kwa kutembelea ofisi ya Katibu wa Jimbo.

    Wakalimani walio kwenye orodha hii wameidhinishwa kutoa huduma katika afisi mahususi za Katibu wa Jimbo na hawaruhusiwi kutoza ada.

    Ili kuomba nakala ya orodha ya wakalimani walioidhinishwa kabla, tembelea ofisi ya Katibu wa Jimbo au tuma barua pepe kwenda MDOS-Access@Michigan.gov.

    Wakalimani wa mara moja

    Iwapo ungependa mtu fulani akutafsirie kwa niaba yako kwa ajili ya majaribio, usikilizaji wa shauri, au kuchunguzwa upya, atapaswa kutuma ombi la kufanya kazi kama mkalimani wa mara moja. Mkalimani wako wa mara moja lazima aidhinishwe na Idara kabla ya ziara yako iliyopangwa na anaweza tu kutoa huduma ya ukalimani kwa ajili ya majaribio, usikilizaji wa shauri lako, au kuchunguzwa upya.
    Ili kutuma maombi ya kuwa mkalimani wa mara moja, mtu huyo lazima:

    • Ajaze na asaini Ombi la Kutoa Huduma za Ukalimani wa Kujitolea, akichagua kwamba atafanya kazi kama mkalimani wa mara moja
    • Atoe picha au nakala ya leseni ya udereva au kitambulisho chake halali ambacho muda wake haujaisha

    Tuma kwa njia ya barua, faksi au barua pepe hati zote zinazotakiwa kwenda:
    Michigan Department of State
    Enforcement Division
    P.O. Box 30708
    Lansing, MI 48909
    Faksi: 517-335-3241
    Barua pepe: SOS-OIS@Michigan.gov

    Mara baada ya idara kupitia maombi, wafanyakazi watawasiliana na mwombaji ili kumjulisha pindi atakapoidhinishwa kutoa huduma za mkalimani wa mara moja.
    Ombi la Kutoa Huduma za Ukalimani wa Kujitolea

     

    Ombi la Kutoa Huduma za Ukalimani wa Kujitolea

  • Ofisi zote za Katibu wa Jimbo hutoa majaribio yaliyotafsiriwa kwa ajili ya mitihani ya maarifa ya udereva katika lugha zifuatazo:

    • Kialbania
    • Kiarabu
    • Kichina
    • Kidari
    • Kiingereza
    • Kifaransa
    • Kigiriki
    • Kihindi
    • Kiitaliano
    • Kijapani
    • Kikorea
    • Kipashto
    • Kipolandi
    • Kireno
    • Kirusi
    • Kihispania
    • Kiukreni
    • Kivietinamu

    Mitihani ya uidhinishaji wa dereva, baiskeli moto, pikipiki, na burudani (Double R) pia hutolewa kwa lugha zifuatazo katika ofisi za Katibu wa Jimbo:

    • Kiingereza
    • Kihispania
    • Kiarabu

     

     

    Taarifa za Leseni na Kitambulisho

     
  • Miamala mingi sasa inaweza kukamilishwa mtandaoni, ikiwemo uhuishaji wa bamba la gari, leseni ya udereva au uhuishaji wa kitambulisho cha jimbo, na ombi la nakala mbili za hati miliki. Kwa kutumia kipengele cha kutafsiri kiotomatiki kwenye kivinjari chako, unaweza kufikia tovuti yetu na kukamilisha miamala ya mtandaoni katika lugha unayopendelea. Tembelea ukurasa wa awali ili kuangalia maelekezo ya kutafsiri kiotomatiki kwenye tovuti ya Idara ya Jimbo.

    Nenda kwenye Huduma za Mtandaoni

  • Tembelea kituo cha kujihudumia ili kuhuisha usajili wa gari lako, nembo na bamba la gari au kuhuisha leseni au kitambulisho chako, ikiwa picha mpya haihitajiki. Vituo vyote 160 vya kujihudumia vya Katibu wa Jimbo vinatoa huduma iliyotafsiriwa katika lugha zifuatazo:

    • Kiarabu
    • Kibengali
    • Kiingereza
    • Kifaransa
    • Kimandarini
    • Kipashto
    • Kihispania
    • Kivietinamu

    Ada ya huduma ya $3.95 itatozwa kwa kila bidhaa itakayotumika kwenye kituo cha kujihudumia.

    Tafuta kituo cha kujihudumia

  • Miamala mingi ya Katibu wa Jimbo inaweza kukamilishwa mtandaoni au kwa barua. Miamala mingi ya leseni ya udereva na vitambulisho na miamala mingi ya kuhuisha nembo ya gari inaweza kukamilishwa kwenye kituo cha kujihudumia. Iwapo utahitajika kutembelea afisi ya Katibu wa Jimbo, unahimizwa sana kupanga ziara ya ofisi. Ziara zinaweza kupangwa hadi miezi sita kabla au siku inayofuata. Maelfu ya ziara za ofisi hupatikana kila siku ya kazi (Jumatatu-Ijumaa) saa 2 asubuhi na saa 6 mchana kwa siku ya kazi inayofuatia.  

    Ili kupanga ziara mtandaoni  kwa lugha unayopendelea, hakikisha unatumia kivinjari ambacho kina kipengele cha tafsiri ya kiotomatiki. Au, panga ziara ya ofisini kwa kupiga simu 888-SOS-MICH (888-767-6424). 


    Au panga ziara ya kutembelea ofisini

    Vinjari tafsiri - Huduma za lugha

     

Chaguzi na taarifa za mpiga kura

  • Unaweza kujisajili kupiga kura Michigani ikiwa:

    • Wewe ni raia wa Marekani 
    • Una angalau umri wa miaka 17.5 (kujiandikisha kabla ukiwa na miaka 16)
    • Kwa sasa hutumikii kifungo jela au gerezani
    • Wewe ni mkazi wa Michigan

    Angalia hali yako ya usajili 

    Kwa kutumia kivinjari chenye kipengele cha kutafsiri kiotomatiki, unaweza kuangalia hali yako ya usajili wa mpiga kura kwenye Michigan.gov/Vote
    Jinsi ya kujisajili

    Unaweza kujisajili ili kupiga kura mtandaoni (ukiwa na leseni na namba ya kitambulisho cha Michigan) au kwa barua hadi wiki 2 kabla ya Siku ya Uchaguzi. Unaweza pia kujisaji moja kwa moja kwenye ofisi ya karani wa eneo lako muda wowote kabla na hadi saa 2 usiku Siku ya Uchaguzi. 

    Huna haja ya leseni au kitambulisho cha Michiganili ili kujisajili kupiga kura kwa barua au kwenye ofisi ya karani wa eneo lako na badala yake unaweza kutoa tarakimu nne za mwisho za namba yako ya Hifadhi ya Jamii. 

    Tafadhali kumbuka kwamba ndani ya siku 14 baada ya uchaguzi, ni lazima ujisajili moja kwa moja kwenye ofisi ya karani wako ukiwa na uthibitisho wa ukazi wako.

    Jisajili mtandaoni: Tumia kivinjari chenye kipengele cha tafsiri kiotomatiki ili kupata usajili wa mpiga kura mtandaoni kwa lugha unayopendelea kwenye Michigan.gov/Vote

    Unaweza kujisajili mtandaoni ikiwa:

    • Una kitambulisho au leseni halali ya udereva ya jimbo la Michigan 
    • Unafahamu tarakimu 4 za namba yako ya Hifadhi ya Jamii 
    • Una angalau umri wa miaka 17.5 
    • Hauko ndani ya siku 14 za Siku ya Uchaguzi 

    Ukijisajili mtandaoni ndani ya siku 14 baada ya uchaguzi au siku ya uchaguzi, hutatimiza vigezo vya kupiga kura katika uchaguzi huo. Usajili wa mtandaoni hauruhusiwi ndani ya siku 10 baada ya kuboresha kitambulisho au leseni yako ya udereva.

    Jisajili mtandaoni

    Tafsiri ya kivinjari – Huduma za lugha
     
    Jisajili kwa kutumia fomu ya usajili inayoweza kuchapishwa: Unaweza kujisajili kupiga kura kwa kutumia fomu ya kujisajili kupiga kura iliyotafsiriwa na inayoweza kuchapishwa. Unaweza kujisajili kwa kutumia fomu ya kujisajili iliyochapishwa ikiwa: 

    • Una Kitambulisho au Leseni halali ya Udereva ya Michigan au una tarakimu 4 za mwisho za namba yako ya hifadhi ya jamii (kimoja tu kinahitajika).
    • Una angalau umri wa miaka 17.5 
    • Hauko ndani ya siku 14 za Siku ya Uchaguzi 

    Fomu ya kujisajili kupiga kura inayoweza kuchapishwa 
     
    Jisajili kwenye kituo cha kujihudumia: Kituo cha kujihudumia hushughulikia usajili wa mpiga kura kwa lugha ambazo si Kiingereza. Tazama sehemu ya Kituo cha Kujihudumia katika ukurasa huu wa tovuti kwa taarifa zaidi.

    Jisajili moja kwa moja kwenye ofisi ya karani wako: Unaweza kujisajili moja kwa moja kwenye ofisi ya karani wa eneo lako. Ndani ya siku 14 za Uchaguzi, lazima ujiasajili moja kwa moja kwenye ofisi ya karani wa eneo lako na lazima uonyeshe uthibitisho wa ukazi. Uthibitisho wa ukazi ni hati rasmi inayotaja jina lako na anwani yako ya sasa, na inaweza kujumuisha taarifa za benki, leseni ya udereva au kitambulisho halali cha MI, mkataba wa upangaji, au bili ya huduma za umma. 
     
    Mtafute karani wa eneo lako

    Kupiga kura kwenye uchaguzi

    Kupiga kura kwenye uchaguzi, lazima uwe:

    • Mpiga kura wa Michigan aliyesajiliwa
    • Una umri wa angalau miaka 18
    • Kwa sasa hutumikii kifungo jela au gerezani 
    • Mkazi wa jiji, kitongoji, au kijiji kile kile cha Michigan kwa angalau siku 30 kabla ya uchaguzi

    Una haki ya kupiga kura ya siri. Ukiwa kama mpiga kura wa Michigan, unaweza kuomba na kupiga kura kwa kutumia kura ya mtu ambaye hayupo katika uchaguzi wowote bila kutoa sababu. 

     
  • Kuomba Kura ya mtu ambaye hayupo

    Kila mpiga kura aliyejisajili Michagan anaweza kupiga kura kwa kutumia kura ya mtu ambaye hayupo. Ili kuomba kutumia kura ya mtu ambaye hayupo, unaweza kujaza na kuwasilisha Ombi la Kura ya Mtu Ambaye Hayupo. 

    Machaguo ya kukamilisha Ombi la Kura ya Mtu Ambaye Hayupo:

    • Kamilisha na uwasilishe ombi mtandaoni kwa kutumia kivinjari chenye kipengele cha kutafsiri kiotomatiki. Omba mtandaoni kwenye Michigan.gov/Vote.
    • Mpigie simu karani wa jiji au mji wako na uombe kutumiwa ombi lililochapishwa kwa njia ya barua. Tafuta ofisi ya karani wa eneo lako kwenye Michigan.gov/Vote.
    • Pakua ombi linaloweza kuchapishwa, lililotafsiriwa ambalo utalirudisha kwa njia ya barua au moja kwa moja kwa karani wa eneo au mji wako. Fomu zilizotafsiriwa zinapatikana kwenye kiungo hiki.
    • Moja kwa moja kwenye ofisi ya karani wa eneo lako iliyoteuliwa.

    Maombi yaliyokamilishwa lazima yapokelewe na karani uliyemchagua kwa njia ya barua, barua pepe au uyapeleke mwenyewe kabla ya saa 11:00 jioni Ijumaa kabla ya Siku ya Uchaguzi.

    Kujaza na kurudisha kura yako ya mtu ambaye hayupo

    Baada ya kutuma maombi yaliyokamilika, kura itatumwa kwenda kwenye anwani yako. Sanduku lako la kura la mtu ambaye hayupo linaweza kutolewa moja kwa moja pindi unapotembea ofisi ya karani wa eneo lako aliyeidhinishwa ndani ya siku 40 za siku ya uchaguzi. 

    Rudisha sanduku la kura la mtu ambaye hayupo mtandaoni au kwa mkono kwa karani wa jiji, mji au kijiji chako kabla ya saa 2 usiku Siku ya Uchaguzi. Huduma za posta za malipo ya awali hutolewa kwa ajili ya kurejesha kura kwa urahisi na bila gharama.

    Machaguo ya kurudisha kura iliyokamilika bila kuwepo kwa wapiga kura:

     

    Ombi la kura ya AV la mtandaoni

    Ombi la kura ya AV linaloweza kuchapishwa

    Mtafute karani wa eneo lako na eneo la sanduka barua

     

    Kupiga Kura Mapema Moja kwa Moja

    Kupiga kura mapema Michigan

    Wapiga kura wa Michigan wana haki ya kupiga kura mapema na moja kwa moja katika eneo la kupiga kura mapema kabla ya Siku ya Uchaguzi.

    Kupiga Kura Mapema kutaanza na uchaguzi wa awali wa rais mwaka 2024 na uchaguzi wa kila jimbo na serikali kuu baadae.

    Ukiwa kama mpiga kura aliyesajiliwa Michigan, una haki ya kuja na mkalimani kwenye eno la kupiga kura mapema. Unaweza kumwomba mtu yoyote kuwa mkalimani, isipokuwa watu wafuatao:

    1. Mwajiri wako
    2. Wakala wa mwajiri wako
    3. Afisa au wakala wa chama chako cha wafanyakazi

    Lini Upige Kura Mapema

    Kipindi cha kupiga kura mapema hutokea kwa siku tisa mfululizo, na zinaisha Jumapili kabla ya uchaguzi. Wanajamii wanaweza kuamua kutoa siku zaidi za kupiga kura mapema, mpaka jumla ya siku 29.

    Vituo vya kupiga kura mapema lazima viwe wazi angalau saa nane kila siku wakati wa kipindi cha kupiga kura ya mapema.

    Kupiga kura mapema hutolewa katika chaguzi zote za majimbo na serikali kuu. Wanajamii wanaweza kuamua kutoa siku za kupiga kura mapema kwa chaguzi za eneo.

    Maeneo ya vituo vya kupiga kura mapema, tarehe, na muda vitapatikana siku 60 kabla ya Siku ya Uchaguzi kwenye Michigan.gov/Vote.

    Mahali pa Kupiga Kura Mapema

    Wapiga kura wanaweza kutembelea vituo vya kupiga kura mapema kwenye maeneo yao ili kupiga kura moja kwa moja wakati wa kipindi cha kupiga kura ya mapema. Eneo la kupiga kura mapema ni kama sehemu ya kupigia kura ambako wapiga kura hupiga kura kabla ya Siku ya Uchaguzi, wakati wa kipindi cha kupiga kura mapema. Wapiga kura wanaotoka maeneo zaidi ya moja ya jiji au mji wanaweza kupangiwa kituo kimoja, au eneo la pamoja la kupiga kura mapema.

    Wapiga kura wanaweza kuangalia maeneo waliyopangiwa ya kupiga kura mapema mapaka siku 60 kabla ya Siku ya Uchaguzi kwenye Michigan.gov/Vote.

     

  • Kupiga kura katika eneo lako la uchaguzi 

    Unaweza kupiga kura moja kwa moja katika Siku ya Uchaguzi kwenye eneo lako ulilochagua kupigia kura. Vituo hufunguliwa kati ya saa 1 asubuhi na saa 2 usiku kwa kila uchaguzi. Ikiwa uko katika mstari wa kupiga kura saa 2 usiku wakati upigaji kura unafungwa, bado unaweza kupiga kura na unahimizwa kusalia kwenye foleni ili kupokea kura yako. 

    Ukiwa kama mpiga kura aliyesajiliwa Michigan, una haki ya kuja na mkalimani kwenye uchaguzi. Unaweza kumuomba mtu yoyote kuwa mkalimani, vinginevyo ni watu ambao wanaweza kushawishi kura yako. Mkalimani wako hawezi kuwa: 

    1. Mwajiri wako
    2. Wakala wa mwajiri wako
    3. Afisa au wakala wa chama chako cha wafanyakazi

    Ili kujua kituo chako cha kupiga kura, tembelea  Michigan.gov/Vote

     

     Nenda kwenye Michigan.gov/Vote

     

  • Kwa kutumia kivinjari chenye kipengee cha kutafsiri kiotomatiki, unaweza kuangalia hali ya usajili wa mpiga kura kwenye Michigan.gov/Vote

    Tafsiri ya Kivinjari – Huduma za Lugha

     
  • Simu ya Msaada wa Ulinzi Dhidi ya Vitisho kwa Wapiga Kura & Uchaguzi

    Wapiga kura wana haki ya kupiga kura bila vitisho. Ni kinyume cha sheria kuingilia haki ya mpiga kura kupiga kura. Tumia Simu ya Msaada wa Ulinzi wa Uchaguzi ili kuripoti vitisho kwa mpiga kura.

    Vitisho kwa mpiga kura vinaweza kujumuisha, lakini sio tu: 

    • Watu ambao si wafanyakazi wa uchaguzi au maafisa wa uchaguzi ambao huwaomba wapiga kura hati binafsi
    • Kupiga picha au video wapiga kura bila idhini yao
    • Kuzuia mlango wa kuingilia eneo la kupiga kura, ofisi ya karani, au sanduku la kura la mpiga kura ambaye hayupo
    • Kuuliza maswali au kuwabughudhi wapiga kura
    • Kutoa taarifa uongo au upotoshaji za uchaguzi

    Iwapo utakabiliwa na matatizo yoyote ya kupiga kura yako siku ya kupiga kura au kabla ya Siku ya Uchaguzi, au ikiwa una maswali kuhusu mchakato wa kupiga kura, piga Simu ya Msaada wa Ulinzi wa Uchaguzi kwa msaada:

    • Kiingereza: 866-OUR-VOTE (866-687-8683) 
    • Kihispania: 888-VE-Y-VOTA (888-839-8682) 
    • Kiarabu: 844-YALLA-US (844-925-5287) 
    • Kibengali, Kikantoni, Kihindi, Kikorea, Kimandarini, Kitagalog, Kiurdu, na Kivietinamu: 888-API-VOTE (888-274-8683)

    Huduma za lugha

    Wakazi wa Michigan wana haki ya kuja na mkalimani asiyeongea Kiingereza kwenye ofisi ya karani, kwenye eneo la kupiga kura mapema, au kwenye uchaguzi kwa msaada wa kupiga kura. Mkalimani wako hawezi kuathiri kura yako, hawezi kuwa mwajiri wako, wakala wa mwajiri wako, au afisa au wakala wa chama chako cha wafanyakazi.

    Hakuna utambulisho wa picha unaohitajika

    Ikiwa huna kitambulisho chenye picha, bado unaweza kupiga kura.

    Hakuna sababu za upigaji kura wa mtu asiyekuwepo

    Kila mpiga kura aliyesajiliwa katika jimbo la Michigan ana haki ya kutumia kura ya mtu ambaye hayupo ili kupiga kura akiwa nyumbani, kupiga kura mapema au kupiga kura kwa barua. Pata maelezo zaidi katika kiungo hiki.

    Uandikishwaji wa mpiga kura siku hiyo hiyo

    Wakazi wa Michigan wanaostahiki wanaweza kujiandikisha kupiga kura Siku ya Uchaguzi kwa kutembelea ofisi ya karani aliyeteuliwa na kutoa uthibitisho wa ukazi wao. Uthibitisho wa ukjazi ni hati rasmi yenye jina na anwani yako ya sasa, na inajumuisha (lakini sio tu) Leseni ya Udereva au Kitambulisho cha Jimbo, bili ya huduma za umma, taarifa ya benki au kadi ya mkopo, au hundi ya malipo. Pata maelezo zaidi kwenye Michigan.gov/VoterRegistration.

    Raia wanaorejea

    Hapa Michigan, raia wanaorejea, au watu ambao walifungwa hapo awali, bado wanastahiki kujisajili kupiga kura, hata kama wapo kwenye msamaha au uangalizi. Mtu ambaye yupo jela kabla ya hukumu au anasubiri hukumu anastahiki kujisajili na kupiga kura ya mtu ambaye hayupo. Katazo pekee la kujiandikisha na kupiga kura kwa mtu aliye jela au mahabusu ni kwa wale ambao wamefungwa baada ya kuhukumiwa. Pata maelezo zaidi kwenye Michigan.gov/VoterRegistration.

    Ufikiaji wa mpiga kura

    Wapiga kura wa Michigan wana haki ya kuyafikia maeneo ya kupigia kura na kuvitumia Vituo vya Msaada wa Wapiga Kura (VAT) ili kupata msaada wa kupiga kura. VAT ni vifaa vya kuwekea alama kwenye kura vyenye vitu maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kusikia, kuona, viungo vya mwili na ulemavu mwingine. Wapiga kura wana haki ya kupiga kura kwa uhuru na faragha bila msaada wa kutumia VAT, na wakaguzi wa uchaguzi wa kituoni (wasimamizi wa uchaguzi) wanapatikana ili kutoa msaada au kutoa maelekezo wanapoombwa.

     

     

  • Jamii zifuatazo zinatoa nyenzo za uchaguzi zilizotafsiriwa kwa lugha maalum:

    • Jiji la Dearborn: Kiarabu
    • Jiji la Hamtramck: Kibengali
    • Jiji la Fennville: Kihispania 
    • Mji wa Colfax: Kihispania

    Ukiwa kama mpiga kura aliyesajiliwa Michigan, una haki ya kuja na mkalimani kwenye uchaguzi. Pitia “Haki zako za kupiga kura” mapema kwenye ukurasa huu kwa maelezo zaidi. 

     
  • Ukikabiliwa na matatizo yoyote kupiga kura yako wakati au kabla ya Siku ya Uchaguzi, piga Simu Msaada wa Ulinzi wa Uchaguzi kwa msaada:

    • Kiingereza: 866-OUR-VOTE (866-687-8683) 
    • Kihispania: 888-VE-Y-VOTA (888-839-8682) 
    • Kiarabu: 844-YALLA-US (844-925-5287) 
    • Kibengali, Kikantoni, Kihindi, Kikorea, Kimandarini, Kitagalog, Kiurdu, na Kivietinamu: 888-API-VOTE (888-274-8683) 
     

Fomu na machapisho

Tafuta nyenzo na zana za uchaguzi zilizotafsiriwa kwa kutumia menyu ya Fomu na Machapisho. Chagua lugha unayopendelea kwa kutumia Lugha ili kuchuja muonekano wa hati zote zilizotafsiriwa.

 

Fomu & machapisho

 

Omba nyaraka iliyotafsiriwa

Kuomba hati iliyotafsiriwa, tafadhali tuma barua pepe kwenda MDOS-Access@Michigan.gov Tadhali jumuisha taarifa zifuatazo kwenye ombi lako la kwenye barua pepe:

  • Jina la hati.
  • Lugha iliyoombwa kutafsiriwa.